Friday 6 July 2012

MATOKEO YA MITIHANI YA NBAA - MAY 2012

Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imetoa matokeo ya mitihani iliyofanyika May 2012.

Walio jiandikisha kufanya mitihani hiyo walikuwa 4,315, lakini walio udhuria kwenye vyumba vya mitihani walikuwa 3,857, ikimaanisha kwamba jumla ya wanafunzi 458 waliingia mitini!

Module E ilikuwa na idadi kubwa ya walio jiandikisha kufanya mitihani, na ndio yenye idadi kubwa ya walioingia mitini kwa jumla ya wanafunzi 342, kati ya 458.

Sababu ya idadi kubwa ya wanafunzi katika Module E ni exemption wanayopewa wanafunzi waliomaliza vyuo vinatambuliwa na NBAA. Julma ya vyuo vinavyo tambuliwa na NBAA ni 16.

Walio kamilisha hatua ya mwisho ya (Module F) ni 259, kati yao wanaume ni 183 na wanawake 76. Waliofaulu na kukamilisha ATEC ni 35, kati ya hao wanaume ni 23, na wanawake 12.

Utafiti wa NBAA umeonyesha kwamba, baadhi ya sababu za wanafunzi kutofanya vizuri ni: ukosefu wa vifaa (training materials), lugha ya Kiingereza, kutokuwa na msingi mzuri wa uelewa wa mahesabu, na msongamano wa wanafunzi madarasani.

Kuona matokeo twanga link-
http://www.nbaa-tz.org/examinations/results/may_exams/Results_Summary.htm

No comments:

Post a Comment