Thursday 20 June 2013

VIDEO YA HALI ILIVYOKUWA BAADA YA MLIPUKO VIWANJA VYA SOWETO, ARUSHA

Tukio hili la lilitokea siku ya Jumamosi,15 June 2013 kwenye viwanja vya Soweto, Arusha, kwenye mkutano wa CHADEMA kukamilisha kampeni za udiwani, ambapo watu kadhaa walipoteza maisha.

Tahadhari: Picha zilizo rekodiwa zinatisha.....

Mh MBOWE NA Mh LEMA WAJISALIMISHA KITUO CHA POLISI, WADAI TUME HURU YA UCHUNGUZI

Mh Freeman Mbowe na Mh Godbless Lema walijisalimisha kwenye kituo kikuu cha polisi Arusha, baada ya kutakiwa kufanya hivo, ili kujibu tuhuma za kufanya mkusanyiko wa waombolezaji kwenye viwanja vya Soweto isivyo halali.

Hata hivyo Mh Mbowe alisema hawako tayari kukabidhi ushahidi 'kwa jeshi la polisi kwasababu jeshi la polisi ni watuhumiwa'. Hivyo ameitaka serikali kuunda tume huru ya uchunguzi ambayo inaweza kuundwa na rais.

kujua zaidi twanga link....
http://www.youtube.com/watch?v=h4nXsK5RovA&feature=player_embedded

Wednesday 19 June 2013

LIGI KUU YA UINGEREZA - RATIBA YA MECHI ZA MSIMU WA 2013 / 14

Ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa 2013 / 14 itaanza kwa mechi za ufunguzi tarehe 17 August 2013 na kufikia tamati kwa mechi za kufunga msimu tarehe 14 May 2014.

Timu zilizopanda daraja msimu huu ni Hull, Crystal Palace na Cardif.

Zifuatazo ni mechi za ufunguzi tarehe 17 August 2013:

Aston Villa v Arsenal
Chelsea v Hull City
Crystal Palace v Tottenham
Liverpool v Stoke City
Manchester City v Newcastle
Norwich City v Everton
Sunderland v Fulham
Swansea v Manchester Utd
West Bromwich v Southampton
West Ham Utd v Cardif City

NB: Mechi zote zitaanza saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Kuona ratiba kamili twanga link zifuatazo..

http://www.premierleague.com/en-gb/news/news/2013-14/jun/fixture-list-for-2013-2014-season-released.html

http://metro.co.uk/2013/06/19/201314-premier-league-fixtures-arsenal-manchester-united-chelsea-tottenham-check-out-all-your-teams-dates-in-the-full-fixture-list-and-grid-3847412/

Tuesday 18 June 2013

Mh MNYIKA ASEMA 'USHAHIDI WA VIDEO UMEONYESHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIMEHUSIKA NA TUKIO LA SOWETO, ARUSHA

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Mh Mnyika ametoa kauli juu ya tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye viwanja vya Soweto, jijini Arusha. Pia amezungumzia matukio mengine.

Kuhusu tukio la mlipuko kwenye viwanja vya Soweto Arusha lililotokea Jumamosi, 15 June 2013, Mh Mnyika amedai kwamba, ushahidi wa video umeonyesha kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vimeshiriki katika 'kupanga tukio, kutekeleza tukio la mauaji, kurusha bomu, kufyatua risasi kwa bastola, kufyatua risasi kwa bunduki na vitendo vingine kwenye tukio hilo...'

Mh Mnyika amemuomba rais kuwaeleza Watanzania, 'nini amekifahamu kabla ya tukio, wakati wa tukio, na sasa, kufuatia ushahidi ambao umeonyesha wazi kwamba askari wamehusika katika tukio hilo.

Kusikiliza / kuona twanga link
http://www.youtube.com/watch?v=9Mda0plu1DM&feature=player_embedded#!

WAOMBOLEZAJI WA CHADEMA VIWANJA VYA SOWETO JIJINI ARUSHA WATIMULIWA KWA MABOMU

CHADEMA ilipanga siku hii ya Jumanne, 18 June, kuwa ni siku maalum ya kuombeleza vifo vya watu waliopoteza maisha siku ya Jumanosi, 15 June 2013, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha.

Mlipuko huo ulitokea  wakati CHEDEMA ikihitimisha kampeni za uchaguzi wa madiwani wa kata ya Kaloleni.

Maombolezo nayo yalisitishwa kwa mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi ili kutawanya waombolezaji walio jikusanya kwenye viwanja hivyo vya Soweto.

DSCF9335
Pichani ni sehemu ya tukio, polisi walipofanya kazi yao..



Vizuizi babararani wananchi wakionyesha hisia zao

DSC09343
Pichani: Kulia ni polisi wakilinda doria, na kushoto ni moja ya eneo linalofaniywa uchunguzi kufuatia mlipuko 15 June.

Mikusanyiko katika viwanja vya Soweto ilisitishwa ili kupisha zoezi la uchunguzi kufuatia mlipuko wa bomu siku Jumamosi, 15 June 2013. Viongozi wa CHADEMA walishauriwa kuwafahamisha wafuasi wa chama hicho sehemu tofauti ya kufanyia maombolezo.

Sunday 16 June 2013

MECHI ZA 16 JUNE 2013, NCHI ZA AFRIKA - KUWANIA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA

15:00 Tanzania 2 - 4  Ivory Coast
15:00 Lesotho 0 - 2 Ghana
15:00 Mozambique 0 - 1 Egypt
15:30 Rwanda 0 - 1 Algeria
15:30 Congo DRC 0 - 0 Cameroon
16:00 Ethiopia 2 - 1 South Afrika
17:00 Eq Guinea 1 - 1 Tunisia
17:00 Guinea 2  - 0 Zimbwabwe
18:00 Mali 2 - 2 Benin

NB: Saa za Afrika Mashariki

Taifa Stars shwari sana, ili kusonga mbele lazima ishinde kwenye mechi ya iliyobaki dhidi ya Gambia na kuomba duwa Ivory Coast ishinde dhidi ya Morocco.

Msimamo wa kundi C (point mabanoni): 1.Ivory Coast (13), 2.Morocco (8), 3.Tanzania (6), 4.Gambia (1)

Saturday 15 June 2013

MLIPUKO WA BOMU (AVURUGA MKUTANO WA CHADEMA VIWANJA VYA SOWETO, JIJINI ARUSHA

Mkutano hadhara wa CHADEMA kufunga kampeni za udiwani kata ya Kaloleni, uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, jijini Arusha umeingia dosari kufuatia mlipuko wa bomu, ambapo watu watatu wanadaniwa kupoteza maisha na wengi kujeruhiwa.

   DSC07407??????????????????????
Majeruhi baada ya mlipuko.....

Mkutano huo uliudhuriwa na viongozi wa CHADEMA wakiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Mh Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha mjini, Mh Godbless Lema ambao awakudhurika.

           ??????????????????????
 Viongozi  wa CHADEMA juu ya lorry lililokuwa likitumika kama jukwaa

Mlipuko huo unadaiwa kutokea eneo la jukwaa ambalo viongozi CHADEMA walikuwa wakitumia lakini wakati mlipuko viongozi hao walikuwa wameshuka ili kukusanya michango toka kwa wananchi, hivyo kunusurika na mlipuko huo.

Askari wa kuzuia fujo walifika eneo la tukio na kutumia mabomu ya machozi lakini askari hao walitolewa mkuku na wananchi wenye hasira, nalo gari la wagonjwa lilivunjwa vioo na wananchi kwa kile kinachodaiwa kuchelewa kufika eneo la tukio.

Kwa picha  zaidi twanga link zifuatazo......

-- http://jamiiblog.co.tz/2013/06/15/bomu-lalipuka-arusha-kwenye-mkutano-wa-chadema-watano-waofiwa-kufa-na-wengine-70-wajeruhiwa/

-- http://arusha255.blogspot.co.uk/2013/06/breaking-news-mbowe-lema-asururika.html


Kwa video baada ya mlipuko twanga link.........

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=hUotiwu100g#at=236 


Kwa video ya hotuba za viongozi mpaka wakati wa mlipuko twanga link ifuatayo.....

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=rDEiY2vhFI8#at=13