Sunday 1 July 2012

MECHI YA 01 JULY 2012 - FINAL UEFA EURO 2012

21:45 Spain 4-0 Italy

NB: Saa za Afrika Mashariki

Spain Mabingwa wa EURO 2012

Kipindi cha kwanza kilimalizaka Spain ikiongoza 2-0. David Silva alipata bao la kwanza kwenye dakika ya 14, naye Alba akafunga bao la pili dakika ya 41.

Dakika ya 15 ya kipindi cha pili, Thiago Motta aliyeingia badala ya R.Montolivo alishindwa kuendelea na mchezo kutokana na matatizo ya misuli. Ikiwa imeshatumia wachezaji wote watatu wa akiba, Italy wailazimika kucheza muda uliobakia wakiwa na wachezaji 10.

Huku Italy ikiwa na wachezaji pungufu, Spain wakatumia vizuri msemo wa 'kuvuja kwa pakacha',  kwa kutawala mchezo na kufanikiwa kuongeza bao la tatu dakika ya 84 kupitia Fernando Torres, na dakika nne baaaye Mata akaongeza bao la nne na la mwisho.


----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ni mechi ya fainali kupata mshindi wa UEFA EURO 2012,  Ni Spain ama Italy?

No comments:

Post a Comment