Friday 6 July 2012

R.FEDERER AMSHINDA N.DJOCKOVIC, KUCHEZA FAINALI NA ANDY MURRAY

Bingwa tennis duniani kwa upande wa wanaume, Novak Djockovic, ameshindwa kuonyesha ubabe wake mbele ya Rodger Federer kwenye nusu fainali ya michuano ya tennis ya Wimbledon 2012, nchini Uingereza.

Federer anayeshikilia nafasi ya 3 duniani, amemshinda Djokovic kwa set 6-3, 3-6, 6-4, 6-3.

Ushindi huo umempa Federer nafasi ya kucheza fainali, pia atakuwa ameweka record ya kucheza fainali za Wimbledon kwa mara ya nane.

Naye Mwingereza, Andy Murray (namba 4) amemshinda Mfaransa, J-Wilfred Tsonga (namba 5) kwenye nusu fainali kwa ushindi wa 6-3, 6-4, 3-6, 7-5.

Murray naye amekuwa raia wa kwanza wa UK kufanikiwa kucheza fainali za Wimbledon (single) baada ya miaka 74 kupita. Fred Perry ni raia pekee wa UK, aliyefanikiwa kucheza na kushinda fainali za Wilmbledon za mwaka 1938. 

Kwa matokeo haya, Federer na Murray watacheza fainali siku ya Jumapili, 08 July 2012.

No comments:

Post a Comment