Monday, 16 April 2012

M/KITI WA UV-CCM ARUSHA, JAMES OLE MILLYA AMEHAMIA CHADEMA

Uenda ni mambo ya mfa maji!

Labda sababu kiti cha mbunge Arusha mjini kipo wazi, na wanao kimezea mate waanza kufarakana wenyewe kwa wenyewe.

Wimbi hilo limejitokeza ndani ya CCM ambapo Mwenyekiti wa UV-CCM, James Ole Millya sio tu amejivua wadhifa huo bali amejitoa uanachama wa CCM.

James Ole Millya amechukua uamuzi huo wakati kamati kuu ya CCM mkoa wa Arusha ilikuwa kwenye mchakato wa kutoa uamuzi kufuatia kutoelewana kati ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda na Jame Ole Millya.

James Ole Millya amehamia CHADEMA. Na kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Mbowe amemkaribisha na kutoa wito kwa wana CCM safi kuhamia CHADEMA.

No comments:

Post a Comment