Thursday, 5 April 2012

GODBLESS LEMA (CHADEMA ) AVULIWA UBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI

Ndugu Godbless Lema wa CHADEMA amevuliwa ubunge jimbo la Arusha Mjini aka kiti cha ubunge kipo wazi rasmi!

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha kufuatia kesi ya madai ya kupinga ushindi wa Godbless Lema aliyepata kura 56,596 dhidi ya 37,460 alizopata Batilda Buriani (CCM) kwenye uchaguzi wa 2010. Kwa sasa Batilda Buriani ni balozi wa Tanzania nchini Kenya.

Kesi hiyo ya madai dhidi ya ushindi wa ndugu G.Lema ilifunguliwa na makada wa CCM ambao ni Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo, waliodai kuwa ndugu G.Lema alikiuka taratibu za uchaguzi kwenye mikutano ya kujinadi.

Kufuatia uamuzi huo Godbless Lema anatakiwa kulipa gharama zote za kesi. Hata hivyo inasemakana Ndugu Lema amekubali kutokata rufaa dhidi uamuzi wa mahakama na amesema yupo tayari kugombea upya ubunge huo.

Kufuatia ushindi wa uchaguzi wa ubunge Arumeru Mashariki uliofanyika 01 Apri 2012, ni dhahiri kuwa CHADEMA itanyakua bila wasiwasi marudio ya uchaguzi wa kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini.

 
Pichani: Katikati ni mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Mbowe akiwahutubia wananchi baada ya uamuzi wa mahakama, kushoto ni Mh Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na kulia ni Ndugu Godbless Lema.

Ni dhahiri ndani ya miezi mitatu a.k.a siku 90 wananchi wataamua nani ni mbunge. Tusubiri tarehe ya uchaguzi itangazwe na tume ya uchaguzi?

No comments:

Post a Comment