Saturday 18 August 2012

KWA WALE WANAOISHI UGHAIBUNI - MWONGOZO WA UTOAJI MAONI YA KATIBA MPYA

Unahishi ughaibuni na unapenda kutoa maoni kuhusu upatikanaji wa katiba mpya?

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa mwongozo kuhusu utaratibu wa 'Watanzania wanaoishi Ughaibinu'.

Kwanza, unaijua Katiba Ya Jamuhuri ya Muungano ya Mwaka 1977 na  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, sura ya 83? Zinapatikana hapa www.katika.go.tz

Pili, mambo ya kuzingatia katika utoaji maoni:-

-Mwenye haki ya kutoa maoni ni Mtanzania kwa uraia wake, (ambaye hajapoteza uraia).

-Ukusanyaji maoni ni kwa njia ya: mitandao ya kijamii, barua pepe ya tume, nyaraka / barua ....

-Majina yako matatu, namba ya pasi ya kusafiria na mahali ilipotolewa , nchi na mji unaoishi.

Kwa ufafanuzi zaidi twanga hapa.... http://www.katiba.go.tz/index.php/maoni-nje-ya-nchi

No comments:

Post a Comment