Friday, 21 December 2012

GODBLESS LEMA ASHINDA KESI, SASA NI MBUNGE HALALI....

Godbless Lema (CHADEMA), sasa ni mbunge halali wa jimbo la Arusha Mjini.


 Mh Lema na wafuasi wa Chadema baada ya uamuzi (picha: www.michuzijr.blogspot )

Wanasema 'hakuna kulala mpaka kieleweke', Mh Lema ameshinda rufaa yake dhidi ya hukumu iliyomvua ubunge.

Mh Lema alishinda nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu wa 2010, lakini 05 April 2012 mahakama ya Mjini Arusha ilimvua wadhifa huo baada ya kumkuta na hatia ya kutumia lugha mbofu mbofu kwenye mikutano ya kampeni zake dhidi ya mgombea wa CCM, Matilda Buriani.

Makada wa CCM, Musa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel ndio waliofungua kesi hiyo dhidi ya Mh Lema katika mahakama ya mjini Arusha.

Kufuatia uamuzi huo Mh Lema alikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya mjini Dar es salaam 08 November 2012, alikataliwa na kupewa siku 14 kufanyia marekebisho madai yake na kufanikiwa kusikilizwa 04 December 2012.

Tarehe 21 December 2012, Mahakama ya Rufaa mjini Dar es salaam imepindua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya mjini Arusha na kumrudishia Godbless Lema ubunge wake.

No comments:

Post a Comment