Sunday 6 May 2012

FLOYD MAYWEATHER AMSHINDA MIGUEL COTTO

Floyd Mayweather (35) amembwaga Miguel Cotto(31) kwa Unanimous Decision na kilichobaki ni kwenda jela kutimiza hukumu inayomsubiri.

Pambano hilo la kugombania ubingwa wa light-middleweight (WBA) lilifanyika Jumamosi, 05 May 2012 kwenye ukumbi wa MGM, Las Vegas.

Baada ya kutambiana kwa muda mrefu hatimaye mpambano huo umekamilika na mbabe kupatikana, ambapo waamuzi walimpa Mayweather ubingwa wa point 118-110, 117-111, 117-111 (uninimous decision)

Kwa matokea hayo Mayweather amejiongezea idadi ya ushindi kuwa 43, amepoteza (0 ), kutoka sare (0), wakati Cotto ameshinda mapambano 37, kushindwa (3), kutoa sare (0).

Kuanzia 1 June 2012, Mayweather anatarajiwa kwenda jela kwa miezi miwili kutumikia hukumu (domestic violence), ambayo ilihairishwa ili kumpa nafasi ya kupambana na Cotto.

Baada ya kutumikia hukumu, Mayweather atapambana na nani?  Pacquiao,.. ?


Pambano lingine kali la marudiono ni la Light-Welterweight (WBA na IBF):  19 May 2012- Lamont Peterson v Amir Khan

No comments:

Post a Comment