Monday 27 August 2012

POLISI WAUA MOROGORO, WAVURUGA MAANDAMANO YA CHADEMA

Yale yaliyotokea kwenye maandamano ya Chadema Arusha sasa yamerudiwa Morogoro!

Polisi mjini Morogoro wamemua mtu mmoja kwa jina Ali Zona na kuwajeruhi watu wengine.

Mauaji hayo yamefanywa na polisi waliokuwa wakizuia maandano ya CHADEMA yaliyopangwa kuanzia eneo la Msamvu kuelekea eneo la Kiwanja cha ndege kwa ajili ya mkutano.


 

Inadaiwa CHADEMA ilitaka kufanya mkutano tarehe 08 August 2012 lakini wakazuiliwa ili kupisha sherehe za nanenane, tarehe 25 August 2012 CHADEMA walikubaliana na RPC kwamba mkutano ufanyike 27 August 2012 ili kupisha shuguli za sensa tarehe 26 August 2012.


Inasemekana jioni ya 26 August RPC alisisitiza maandamano yasifanyike bali msafara wa viongozi tu.

27 August 2012 askari polisi wazuia maandamano na kumuua Ali Zona kwa kumpiga risasi kichwa.



Ingawa polisi walitumia nguvu na kusababisha mauaji ili kuzuia maandamano, wananchi waliendele na maandamano na kufika eneo Kiwanja chandege kwa ajili ya mkutano.


http://chademablog.blogspot.co.uk/2012/08/msimamo-wa-john-mnyika-kuhusu-vurugu.html


No comments:

Post a Comment