
Simba SC wakicheza kidedea kushangilia ubingwa
Mbali na kuwacharaza vibaya Yanga, Simba imemaliza mjadala wa ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuchukua rasmi kikombe cha msimu wa 2011-2012.
Mechi hiyo iliyokutanisha miamba hiyo miwili ilifanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Emmanuel Okwi alifanikiwa kuipatia Simba bao la kwanza na la tatu, wakati Felix Sunzu alifunga bao la pili, naye kipa wa Simba Juma Kaseja alipachika bao la nne kwa njia ya penalty na bao la tano lilifungwa na Patrick Mafisango.
Kwa mafanikio hayo Simba imepata ticket ya kushiriki katika kinyang'anyiro cha Ligi ya Mabingwa wa Afrika na mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati msimu ujao.
Azam FC imeshika nafasi ya pili ambapo itashiriki kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao, kikombe ambacho Simba inashiriki msimu huu.
No comments:
Post a Comment