Sunday 6 May 2012

FRANCOIS HOLLANDE ASHINDA UCHAGUZI WA RAIS UFARANSA

Francois Hollande kuwa rais mpya wa Ufaransa baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini humo.

Ushindi wa Francois Hollande umefunga pazia la uongozi wa Nicolas Sarkozy aliyekuwa anagombea
urais kwa awamu ya pili. Sarkozy aliingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2007.

Hollande amezaliwa 12 August 1954, na amekuwa akijishugulisha na mambo ya siasa tangu akiwa mwanafunzi, alijiunga na Socialist Party mwaka 1979.

Kati ya kura zilizopigwa, Hollande ameshinda kwa asilimia 52 wakati Sarkozy alipata asilimia 48,  waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 80.

Francois Hollande anatarajiwa kuapishwa rasmi tarehe 15 au 16 May 2012

No comments:

Post a Comment