Sunday, 13 May 2012

MECHI ZA 13 MAY 2012 - CAF KOMBE LA SHIRIKISHO, SIMBA YATOLEWA KWENYE MASHINDANO

16:00 Black Leopards (S.Africa) 2-0 Warri Wolves FC (Nigeria)
16:30 AC Leopard (Congo) 2-1 Heartland FC (Nigeria)
17:00 Cercle de Bamako(Mali) 3-0 Enppi (Egypt)
19:00 El Amal (Sudan) 0-2 Interclube (Angola)
20:30 C Meknes (Morocco) 0-0 ASEC Mimosas (Ivory Coast)
21:00 Al Ahly Shandi (Sudan) 9-8 Simba(Tanzania)

NB: Saa za Afrika Mashariki

Simba imeinama ikashindwa kuinuka!

Simba imeaga mashindano haya kwa njia ya matuta baada ya A.Shandi kushinda 3-0 na kufanya ngoma kuwa sare kufuatia ushindi wa awali wa Simba 3-0!

Timu zilizosonga mbele ni Warri Wolves, A.C. Leopard, C.Bamako, Interclube, W.Casablanca, C.Africain, C.Meknes, na Al Ahly Shandi.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Ni mechi za marundiano kupata washindi watakao songa mbele kwenye mashindano haya. 

Wydad Casablanca na Club Africain tayari zimefuzu baada ya mechi za 12 May.

Ingawa W.Casablanca imefungwa 1-0 na AS Bamako kwenye mechi ya marudiano, imefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa 3-1  kufuatia ushindi wa mechi ya kwanza. Nayo Club Africain iliifunga Royal Leopard 4-2 na kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa 5-2. 

Simba iliwachabanga Al Ahly Shandi 3-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es salaam, ili kusonga mbele Simba inahitaji angalau matokeo ya sare, ama isifungwe zaidi ya 2-0.

Matokeo mengine ya mechi za kwanza yalikuwa kama ifuatavyo:-

Warri Wolves FC 3-1 Black Leopards, Heartland FC 3-2 AC Leopards, Enppi 3-1 C Bamako, Interclube 4-1 El Amal, ASEC Mimosas 1-1 C Mekens, Wydad Casablanca (Morocco)3-0 AS Bamako (Mali), Royal Leopard (Swaziland) 0-1 Club Africain (Tunisia)

Simba itainama ama itainuka leo?

No comments:

Post a Comment