Monday 3 September 2012

KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI IRINGA, SERIKALI IKEMEE JESHI LA POLISI KUTUMIA NGUVU KUPITA KIASI

Serikali inatakiwa kukemea vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi ili kuepusha vifo, pia jeshi hilo linastahili kupunguziwa mamlaka na kupewa mafunzo zaidi.

Kutumia nguvu kupita kiasi sio suluhisho la matatizo bali inaweza kuwa kichocheo cha vurugu na kusababisa maafa.

Yalizuka Arusha kitambo!  Lakini ni ndani ya wiki moja tangu kutokea Morogoro 27 August 2012 na sasa yamerudiwa Iringa 02 Sept 2012.

Jumapili, 02 September 2012 katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Iringa na mwandishi wa habari wa Channel 10(Iringa) Daudi Mwangosi amefariki dunia baada ya vurugu kuzuka kati ya jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA.


Vifo vinavyotokea haswa katika mikutano ya kisiasa ikiwemo ya CHADEMA, vinaweza kuepukika iwapo jeshi la polisi litatumia busara na mbinu tofauti kuzuia ukiukwaji wa sheria.


Wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika katika ofisi za CHADEMA waliamriwa na polisi kutawanyika lakini waligoma na kuamua kukaa chini.


Pichani chini ni mwili wa Daudi Mwangosi aliyekumbwa na maafa baada ya jeshi la polisi kutumia nguvu kusitisha mkutano wa CHADEMA.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa amesisitiza kwamba, kwa mujibu wa msajili wa vyama vya siasa John Tendwa, mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa nchini imesitishwa mpaka shughuli za sensa zitakapo kamilika 08 September 2012. ( http://www.youtube.com/watch?v=NZZgTiLeLxM&feature=player_embedded#! ) Shughuli za sensa zilianza rasmi 26 August 2012.

Dr Slaa amesema CHADEMA itaendelea na mikutano yake kama kawaida.

No comments:

Post a Comment