Sunday 13 May 2012

PASTOR MALDONALDO ASHINDA SPANISH GRAND PRIX

Pastor Maldonado wa timu ya Williams alianza kwenye nafasi ya kwanza na kumaliza wa kwanza na kushinda Spanish Grand Prix.

Ushindi wa Willams umekuja baada ya miaka 8 kwani ushindi wa mwisho ulikuwa 2004 iliposhinda Brazilian Grand Prix mwaka 2004.

Alonso wa Ferrari ameshindwa kutamba akiwa nyumbani kwa kuambulia nafasi ya pili, akifuatiwa kwa karibu na mkongwe Kimi Raikkonen wa Lotus ambaye alikuwa karibu kuchukua nafasi ya pili kama sio kushinda.

Ngoma ilikuwa kwa Lewis Hamlton aliyeshika nafasi ya 8 tokea nafasi ya 24. Jumamosi Hamilton alishika nafasi ya kwanza kwenye qualifying lakini alipewa adhabu ya kuanza kwenye nafasi ya mwisho (a.k.a 24) baada ya kushindwa kuwa na kiasi cha kutosha cha mafuta.

Mkongwe Michael Schumacher ameendelea kufanya vibaya, safari hii kwa kushindwa kumaliza race baada ya kugonga kwa nyuma Brunno Senna wa Willams na kusababisha Senna kushindwa kumaliza race hizo.

Top 10 ilimalizika ifuatavyo: 1.P Maldonaldo, 2.F Alonso, 3.K Raikkonen, 4 R Grosjean, 5.K Kobayashi, 6. S Vetel, 7.N Rosberg, 8.L Hamilton, 9 J Button, 10.N Hulkenberg 

Matokeo haya yanafanya msimamo wa top 10 kuwa kama ifuatavyo (point mabanoni):
1.Vetel(61), 2.Alonso (61), Hamilton(53), 4.Raikkonen( 49) 5.Webber(48), 6.Botton(45), 7.Rosberg(41), 8.Grosjen(35) 9.Maldonaldo(29), 10.Perez(22)

Race zinazofuata: Monaco Grand Prix , 25 May. 

No comments:

Post a Comment