Tuesday 24 April 2012

MECHI ZA 24 APRIL 2012 - UEFA LIGI YA MABINGWA

21:45 Barcelona 2-2 Chelsea

NB: Saa za Afrika Mashariki

Chelsea wameingia fainali kwa jumla ya ushindi wa 3-2, kwani kwenye mechi ya kwanza walishinda 1-0.  Wanasubiri mshindi wa kesho kati ya Bayern na Real Madrid.

Barcelona walijipatia bao la kuongoza dk ya 35 (Sergio), kwenye dakika ya 36 mlinzi wa Chelsea, Terry alipewa red card. Barcelona wakaongeza bao la pili dk ya 43 (Iniesta), nao Chelsea wakapachika bao la kwanza kabla ya mapumziko dk45 (Remires).

Katika kipindi cha pili Barcelona walitawala mchezo, Chelsea nao walilinda eneo la goli muda mwingi, na hatimaye Torres alichomoka na kuipatia Chelsea bao la 2 dakika ya mwisho na kuwamaliza nguvu Barcelona.

Barcelona watajilaumu kwa kukosa penalty (Messi) na kushindwa kuipangua safu ya ulinzi ya Chelsea.

KUJUA yaliyojiri kwenye Ligi kuu ya Uingereza angalia hapo juu!

--------------------------------------------------------------------------------------------------
Ni Nusu fainali mechi ya marudiano, ambapo mechi ya awali Chelsea walishinda 1-0. Lakini Chelsea hawana uhakika wa kucheza kwenye Ligi hii ya Mabingwa msimu ujao, kutokana na kuvurunda kwenye Ligi kuu ya Uingereza, hivyo uenda watalinda ushindi wao wa awali kwa udi na uvumba ili kuhakikisha wanafika fainali. 

Barcelona wamepoteza mechi mbili zilizopita, kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea (1-0) na kwenye Ligi kuu ya Spain dhidi ya Real Madrid (2-1). Tofauti na Chelsea, Barcelona wanacheza mechi hii wakiwa na uhakika wa kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao, kwani watamaliza ligi ya Spain wakiwa kwenye nafasi ya kwanza ama ya pili.

Chelsea wakae mkao, wakumbuke yaliyo watokea Arsenal!

No comments:

Post a Comment