Sunday 1 April 2012

UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI - 01 APRIL 2012

Wanasema 'hakuna marefu...............'

Watu wamepanda na wengine wameshuka, vifijo na kelele zimepigwa na wengine wamelalama kwa muda mrefu.

Ni siku ya uchaguzi mdogo wa mbunge wa Jimbo Arumeru Mashariki kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jeremiah Sumari (CCM).

Katika uchaguzi wa 2010 jumla ya kura 55,698 zilizopigwa matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Jeremiah Sumari (CCM) alipata kura 34661 ( 62.23 %), Joshua Nassari alipata kura 19123 (34.33%). John Pallangyo (CUF) kura 265 (0.48%), Linda Bana (Jahazi Asilia) kura 176 (0.32%), Fannuel Pallangyo (TLP) kura 88 (0.16%), Charles Msuya (UPDP) kura 88 (0.16%), na kura 1297 ziliharibika.

Katika uchaguzi wa leo kuna wagombea 8 wa kiti cha hicho cha ubunge kama ifuatavyo (vyama mabanoni):-

Sioyi Sumari (CCM)
Joshua Nassari (CHADEMA)
S.Moyo (SAU)
Charles Msuya (UPDP)
Abraham Chibaka (TLP)
Abdalah Mazengo (AFP)
Mohamed Mohamed (DP)
Khamis Kihemu (NRA)

Jumla ya vituo vya kupigia kura ni 327, ambapo wapiga kura ni 127,455 ikiwa ni ongezeko la wapiga kura 26 ukilinganisha na idadi ya wapiga kura kwenye uchaguzi wa 2010

Je watajitokeza wapiga kura wangapi? Nani atashinda na kwa asilimia ngapi? Nani atalalama na kwa vigezo gani?

No comments:

Post a Comment