Sunday 1 April 2012

CCM YAJITOA KWENYE UCHAGUZI MDOGO ARUMERU MASHARIKI

Kinyume na matarajio ya wengi, hatimaye CCM imepitisha uamuzi wa kujitoa kwenye mbio za kugombea kiti cha ubunge wilaya ya Arumeru Mashariki.
Sababu kubwa za kufikia uamuzi huo ni pamoja na utata wa uraia wa mgombea wa CCM,  pia chama hicho kuhisi kutoweza kupata ushindi uliotarajiwa hapo awali kufuatia ushindani mkali uliotolewa na CHADEMA.

Hatua hizi uenda zikanufasha chama cha CUF, kwani inategemewa wafuasi wa mgombea wa CCM watamuunga mkono mgombea wa CUF kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya vyama hivyo viwili, swala ambalo si la kushangaza kwani wataalamu wa mambo ya kisiasi nchini wanahisi CUF ni sehemu ya CCM.

CHADEMA imelaani hatua ya CCM kijitoa katika wakati huu, kwani ni kama kuipa CUF ushindi kinyume na matarajio ya wengi waliodhani kwamba ushindani ungeiwezesha CHADEMA kuibuka na ushindi.

Ufuatiliaji zaidi unaendelea ili kuthibitisha utata huu............

NB: Topic hii ilifungwa rasmi saa 4 asubuhi ( unajua tena leo tarehe 01 April) , tazama habari ifuatayo hapo juu kuhusu uchaguzi huu.

No comments:

Post a Comment