Ni uchaguzi wa rais nchini Russia leo ambapo waziri mkuu, Vladimir Putin anashiriki baada ya kufanikisha mabadiliko ya katiba yaliyo mwezesha kugombea urais kwa mara ya tatu.
Putin aliyewahi kuwa rais mwaka 2002-2008, anakabiliwa na upinzani mkali tofauti na ilivyokuwa awali. Katika uchaguzi wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2011, wapinzani walidai kwamba uchakachuaji uliwezesha chama cha Putin kupata karibia 50% ya kura zilizopigwa.
Kufuatia lawama hizo Putin aliagiza utumiaji wa webcam kwenye vituo vyote vya kupigia kura ili kudhibiti uchakachuaji, jambo ambalo linadaiwa alitoshi.
Webcam zitakavyo dhibiti uchakachuaji (Tume ya Uchaguzi ya Tanzania inabidi kujifunza)
Wanao wania urais: Vladmir Putin, Gennady Zyuganov, Vladimir Zhirinovsky, Mikhail Prokhorov, Sergey Mironov
Ili kuwa rais mshindi anatakiwa kupata zaidi ya 50%, la sivyo washindi wawili wa kwanza watapigiwa kura upya kupata mshindi. Hata hivyo Putin anategemewa kushinda.
No comments:
Post a Comment