Monday 20 May 2013

Mh JOSEPH MBILINYI (aka SUGU), NA HOTUBA ILIYO SABABISHA KUHAHIRISHWA KWA BUNGE

Jana, Jumapili, 19 May 2013 ilikuwa siku ya mbunge wa Iringa mjini, Mh Peter Msigwa, leo ni zamu ya mbunge wa Mbeya Mjini, Mh Joseph Mbilinyi aka Sugu.

Mh Mbilinyi, Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, aliwasha moto bungeni kupitia hotuba yake, hali iliyomfanya Spika Anna Makinda kushindwa kuvumulia na kulazimika kuhahirisha kikao cha bunge kwa madai kwamba hotuba hiyo ni ya uchochezi na inakikuka taratibu!!

Katika Hotuba hiyo, Mh Mbilinyi aliishutumu serikali ya CCM kwa madai mbalimbali ikiwemo unyanyasaji wa waandishi wa habari, hali inayoifanya Tanzania kushika nafasi ya 7 kati ya nchi 20 ambazo ni nchi vinara katika unyanyasaji huo duniani, .....

'Mheshimiwa Spika, 

Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!


Kusikiliza hotuba hiyo kwa masikio yako na kujua uwazi usiofichika twanga link......... 
http://www.bongo5.com/in-case-umemiss-kauli-ya-sugu-iliyosababisha-bunge-lisitishwe-ghafla-leo-kuogopa-uchochezi-audio-05-2013/

Kusoma hotuba kamili twanga link hii- http://chademablog.blogspot.co.uk/2013/05/msemaji-mkuu-wa-kambi-ya-upinzani.html

No comments:

Post a Comment