Baada ya kusuasua katika mchakato wa kupata mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki, hatimaye jana 03 Mar 2012, CCM imempitisha Siyoi Sumari kugombea uchaguzi utakaofanyika 01 April 2012.
Kama Sumari atafanikiwa kupata kiti hicho cha ubunge, itaendeleza 'mbio za kupokezana vijiti' a.k.a mfano wa viongozi wa CCM kurithishana madaka kwenye familia zao, pindi mmoja anapotoka madarakani. Hata hivyo wapiga kura ndio wanao hitajika kuleta mabadiliko kwenye swala hili, kwa kuwachagua wagombea wenye sifa zinazotakiwa.
Sumari atapata ushindani mkubwa toka kwa mgombea wa CHADEMA, Joshua Nasari ambaye uenda akaungwa mkono na wafuasi wa wagombea wa CCM walioshindwa kwenye kura za maoni.
Kwenye kura za maoni ndani ya CCM, Siyoi Sumari alipata kura 761 kati ya 1122. Wakati kwenye kura za maoni ndani ya CHADEMA, Joshua Nassari alipata kura 805 kati ya kura 888. Kwa mtazamo hiyo ingekuwa idadi kamili ya wapiga kura tarehe 1April, alafu CHADEMA waungwe mkono na wapiga kura 361 (i.e 1122- 761) wa CCM, basi mambo yasinge kuwa shwari kwa mgombea wa CCM! Hata hivyo idadi ya wapiga kura itakuwa tofauti kama sio kubwa.
No comments:
Post a Comment