15:45 Liverpool 1-2 Arsenal
18:00 Blackburn 1-1 Aston Villa
18:00 Man City 2-0 Bolton
18:00 QPR 1-1 Everton
18:00 Stoke 1-0 Norwich
18:00 West Brom 1-0 Chelsea
18:00 Wigan 0-2 Swansea
NB: Saa za Afrika Mashariki
Arsenal wapewe nini tena? Kama kuna game la kushinda na kupata point 6 ni hapo Tottenham atakapopigwa na Man Utd kesho, labda isiwe hivyo! Arsenal wananyemelea nafasi ya tatu kwa nguvu zote.
Kushindwa kwa Chelsea kweli ni dalili za kuyumba kwa jahazi, matokeo hayo ni zawadi kubwa kwa Arsenal inayofukua vumbi na kuiacha Chelsea kwa point tatu.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kindumbwe ndumbwe leo! Mabingwa wa kombe la Carling, Liverpool wanashikilia nafasi ya 7 kwa point 39, ikishinda leo itabaki nafasi ya 7 lakini itaongeza matumaini ya kumaliza top four.
Arsenal inashikilia nafasi ya 4 kwa point 46, wanahitaji ushindi ikiwa ni jitihada za kunyemelea nafasi ya 3, inayoshikiliwa na Tottenham yenye point 53. Pia ushindi utamthibitishia Wenger kwamba yeye kweli ni manager bora wa mwezi wa Feb.
Vinara wa ligi hii Man City ina point 63, ushindi wa leo utawaacha ManUtd kwa tofauti ya point 5, kupoteza mechi hii itawapa mwanya Man Utd kuchungulia nafasi ya kwanza kama ikishinda kesho dhidi ya Tottenham. Bolton wanaitaji ushindi ili kuepuka janga la kushuka daraja!
Chelsea iliyopo nafasi ya 5 ina point 46 sawa na Arsenal, hivyo kuteleza kwa Arsenal itakuwa sherehe kwa Chelsea kama itashinda. Kushindwa leo kwa Chelsea leo sio tu kutathibitisha usemi wa Lampard kwamba kuna kutoelewana kati yake manager wao Villas-Boas, bali hali si shwari Chelsea nzima.
No comments:
Post a Comment