Uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki unatarajiwa kufanyika tarehe 1 April 2012, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Jeremia Sumari.
Ikiwa leo ni tarehe 1March 2012, CHADEMA imeshateua mgombea wake, bwana Joshua Nassari ili kushiriki kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kufanyika kwa kura za maoni ndani ya chama hicho, ambapo J.Nassari alipata kura 805 kati ya kura 888 zilizopigwa.
CCM wanasuasua kukamilisha kura za maoni ndani ya chama hicho leo ikiwa ni hatua za kumpata mgombea wao, mchakato ambao umeanza kugubikwa na kashfa za rushwa.
Wagombea wengine watakuwa kina nani, na nani atashinda? Tufuatilie ........
No comments:
Post a Comment