Wednesday, 8 February 2012

SIASA NA MAISHA YA WAGONJWA KIPI BORA?



Pichani Mh Rais Kikwete alipokutana na wawakilishi wa wamachinga mjini Mwanza tarehe 6 Feb 2012. Wawakilishi hao walieleza mambo mbalimbali wanayo kabiliana nayo.

Mh Rais aliwakabidhi 10 million, kwa ajili ya kukopeshana. Hii ni dalili nzuri na changamoto kwa Wabunge (aka wazee wa Posho) , Mawaziri na viongozi wengine kwamba wanapaswa kujali wananchi wao.

Swali linakuja, kwanini msaada huo uliambatana na sherehe za CCM, na kwanini wamachinga wa Mwanza? Sijasema eti sababu Mwanza ni ngome ya upinzani, kwahiyo kila njia inatumika kuteka moiyo ya wananchi hao ili wabadili mwelekeo kuelekea CCM! HAPANA????

Mgomo wa madaktari umedumu kwa muda mrefu, kiasi cha baadhi ya wagonjwa kukosa huduma muhimu za kiafya sababu ya mgomo huo. Hivi inawezekana kwamba Mh Rais hana habari za mgomo wa madaktari, na hali za wagonjwa wanaotaabika ama kupoteza maisha? Labda 10m zingepunguza makali ya maisha kwa madaktari hao na kuokoa maishaa ama mateso ya wagonjwa!

Wakati umefika viongozi wetu kujali maslahi na afya za wananchi wote na kuweka Politiki a.k.a maslahi ya vyama vya siasa pembeni.

No comments:

Post a Comment