Wednesday, 8 February 2012

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA AJIUZULU

Hatimaye Fabio Capello ameachia ngazi kama kocha wa timu ya taifa ya Uingereza,baada ya majadiliano na shirikisho la mpira wa miguu la Uingereza (FA)

Chanzo ni mzozo uliorindima kufuatia uamuzi FA kumvua u captain John Terry, Ijumaa ya wiki iliyopita. Kocha huyo alipinga uamuzi huo na alisisitiza  hayo wakati akihojiwa kwenye television nchini Italy kwa kusema si vyema kwa shirikisho hilo kumuadhibu Captain huyo na badala yake inabidi kusubiri uamuzi wa mahakama.

Pia inadaiwa uenda kocha huyo alichukiwa kwa kutoshirikishwa kwenye uamuzi huo, na alihisi kuingiliwa katika uendeshaji wa timu hiyo. Inasemekana uenda kauli aliyotoa kwenye television ilikiuka mkataba wake!

John Terry anashutumiwa kutoa kauli za ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand wakati wa mechi kati ya Chelsea na QPR mwaka jana. Kesi hiyo ilisomwa kwa mara ya kwanza mahakamani Jumatano ya wiki iliyopita.

Nani atamrithi Fabio? Je Fabio ataondoka mikono mitupu? Shirikisho hilo linatarajiwa kutoa tamko rasmi kesho.

No comments:

Post a Comment