16:30 Arsenal 5-2 Tottenham
16:30 Norwich 1-2 Manchester Utd
18:00 Stoke 2-0 Swansea
NB: Saa za Afrika Mashariki
Hakuna kingine cha kuelezea zaidi ya Arsenal kuisulubisha Tottenham!
Tottenham walianza kwa makeke na kupata bao la kwanza dk ya 4 kufuatia kizunguzungu cha safu ya ulinzi ya Arsenal. Kwenye dk ya 34 Adebayo alipachika penalty na kuifanya Tottenham kuwa mbele 2-0.
Kibao kiligeuka dk ya 40 Sagna alipopachika bao la kwanza kwa kichwa kufuatia cross ya Arteta, na dk 2 baadae Van Parsie akatumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Tottenham na kuipatia Arsenal bao la 2 na timu kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Arsenal wakarudi na nguvu mpya baada ya mapunziko, na baada ya dk 5, Rosicky akapachika bao la 3. Katika dk ya 64 Walcot akapata pass toka kwa Van Parsie na kupachika bao la 4. Hadithi ikaendela Rosicky akatoa pass kwa Van Parie, naye Van Parsie akatoa gonga kwa Walcot naye bila kukosea akapachika bao la 5 kimiani. Mpaka mwisho wa mechi Arsenal wakatoka kifua mbele 5-2
Arsenal wamerudi nafasi ya 4 ikiwa na point 46 sawa na Chelsea iliyoko nafasi ya 5. Tottenham ipo nafasi ya 3 ikiwa na point 53, aka tofauti ya point 7 aka mechi 2 na ushee.!!!
..............................................................................................................................................
Arsenal yenye point 43 inahitaji point tatu kujibu mapigo kwa Chelsea ili kurudi nafasi ya 4, wanapokutana na Tottenham iliyopo nafasi ya 3 na yenye point 53.
Ushindi wa Arsenal sio tu utapunguza kasi ya Tottenham, bali utapunguza majozi ya Arsenal ya kutolewa kwenye kombe la FA baada ya kufungwa na Sunderland 2-0 , bila kusahau kipigo cha 4-0 ilichopewa na AC Milan 4-0 kwenye Ligi ya Machampions wa Ulaya.
Vijana wa zamani wa Arsenal ambao kwasasa wanachezea Tottenham, mshambuliaji Adebayo na mlinzi mahiri Gallas watakutana uso kwa uso na wenzao wa Arsenal, lengo litakiwa ni kupata ushindi na kudhibiti lango la Tottenham. Patakuwa patamu hapoooo!
Norwich yenye point 35 ipo nafasi ya 8. Nao kama walivyo Arsenal wemetolewa kombe la FA, kwa majeraha hayo uenda kazi isiwe rahisi kwa Man Utd ambayo itafanya kila jitihada kuisogelea Man City.
Stoke ipo nafasi ya 14 na Swansea nafasi ya 13, zote zina point 30, hapo ni vuta ni kuvute aka sogea nipite.
No comments:
Post a Comment