Makazi aliyokuwa akiishi Osama bin Laden kwenye mji wa Abbottabad, chini Pakistan yamebomolewa usiku wa jumamosi.
Inadaiwa Osama aliishi katika eneo hilo kwa miaka mingi na familia yake kabla ya kuuliwa. Kikosi maalumu cha jeshi la Marekani kilivamia kwa siri eneo hilo tarehe 2 May 2011 na kuua watu watano akiwemo Osama bin Laden na kisha kuchukua mwili wake na baadae kuuzika baharini.
Kitendo hicho cha jeshi la Marekani kilidhalilisha na kuikasirisha serikali na jeshi la Pakistan kwa kushindwa kugundua uvamizi huo. Pia inasemekana kikosi hicho cha jeshi la Marekani kilivamia eneo hilo bila kuifahamisha serikali ya Pakistan.
Sababu za kubomoa makazi hayo ni kuimarisha usalama katika eneo hilo, kwani makazi hayo yaligeuka kuwa kivutio kwa watu mbalimbali wanaotaka kushuhudia eleo alilokuwa akiishi Osama.
No comments:
Post a Comment