Saturday, 11 February 2012

MECHI ZA 11 FEB 2011 - LIGI KUU YA UINGEREZA

15:45 Man Utd 2-1 Liverpool
18:00 Blackburn 3-2 QPR
18:00 Bolton 1-2 Wigan
18:00 Everton 2-0 Chelsea
18:00 Fulham 2-1 Stoke
18:00 Sunderland 1-2 Arsenal
18:00 Swansea 2-3 Norwich
20:30 Tottenham 5-0 Newcastle

NB: Saa za Afrika Mashariki

Mechi ya Man Utd v Liverpool ilikuwa ya aina yake, kama vile kukwangua madonda,! Kinyongo kuhusu ugomvi wa Suarez na Evra uliozuka mechi ya October 2011, ambapo miamba hii miwili ilikutana na kusababisha na hatimaye Suarez kufungiwa mechi 8 nakutozwa £40,000 kwasababu ya kumtusi Evra kwa maneno ya ubaguzi wa rangi.  Angalia habari inayofuata hapo  juu kujua kituko kilichozuka kati ya Evra na Suarez)

Ushindi wa Man Utd leo umewasogeza nafasi moja juu mpaka kileleni wakiwa na point 58. Liverpool imebakia nafasi ya 7 na  point 39.

Kibano ilichopokea Chelsea kutoka kwa Everton kimewashusha nafasi moja chini mpk nfasi ya 5, wakiwa na point 43 sawa na Arsenal. 

Arsenal wamefanikiwa kuwatwanga Sunderland na kuzoa point tatu na kusogea nafasi mbili  juu mpaka nafasi ya 4, na kuongeza matumaini ya kumaliza msimu ikiwa kwenye top four ili kucheza Ligi ya Machampion wa Bara la Ulaya (UEFA) msimu ujao.

Tottenham wamefanya sherehe ya magoli kwa kuwacharaza Newcastle bila huruma na kiendeleza juhudi za kutaka kumaliza kwenye top four ili kucheza Ligi ya Machampion wa Bara la Ulaya msimu ujao. 

Top 10 ilivyo (point kwenye mabano)
1Man Utd (58), 2.Man City (57),  3.Tottenham (53), 4.Arsenal (43), 5.Chelsea (43), 6.Newcastle (42), 7.Liverpool (39), 8.Norwich (35) 9.Sunderland (33) , 10.Everton (33)

No comments:

Post a Comment