22:00 Ghana 0-2 Mali
NB: Saa za Afrika Mashariki.
Ni mechi ya kupata mshindi wa tatu, ni Ghana ama Mali kuibuka kidedea leo?
Ghana wana hasira kaa mbogo aliyejeruhiwa! Watapunguza munkari kama watajishindia nafasi ya tatu. Kukosa kucheza final na Gyan kukosa penalty ilikuwa pigo kubwa kwa Ghana, na uenda uchezaji wa leo utadhihirisha wazi!
Kwa Mali kushinda nafasi ya tatu , ni kama kupata ubingwa. Ni dhahiri Mali wana matumaini makubwa ya ushindi dhidi ya Ghana.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mali wamedhihirisha kwamba hata wao wanajua kandanda na kuwapiga Ghana mitwango miwili kwa mtungi! Uenda Zambia watafuata nyayo za Mali hapo kesho kwa kuibuka kifua mbele
Final kesho: 22:30 Zambia v Ivory Coast
No comments:
Post a Comment