Luiz Suarez alikwepa bila aibu kitendo cha kupeana mikono kati yake na Evra. Jambo hilo lilimwacha Evra kwenye wakati mgumu huku aking'ang'a mkono wa Suarez. Juhudi hizo ziligonga ukuta hata pale kipa wa Man Utd aliyekuwa anafuatia baada ya Evra akijaribu kumlazimisha Suarez kumpa mkoni Evra. Baada ya kuona tukio hilo kaptain wa Man Utd, Rio Ferdinand naye alikukataa kumpa mkono Suarez na kudhihirisha ule usemi wa 'ukiua kwa upanga.............!
Wakati wa mapumziko nao ulizua utata na kusababisha ulinzi wa ziada utumike ili kuepusha ugomvi uliokuwa unaelekea kuzuka kati ya wachezaji wa timu hizo mbili.
Hata hivyo ingawa Bwawa la maini walishinda kwa kuwa wagomvi katika mechi hiyo, ni Man Utd walioshibuka na ushindi 2-1 na kudhihirisha kwamba mpira ni magoli na sio ugomvi.
Mabao ya Man Utd yalipachikwa na Rooney, wakati bao la Liverpool lilifungwa na Luiz Suarez. Mabao yote yalipatikana kwenye kipindi cha pili. Kwa ushindi huo Man Utd inaongoza ligi kwa point 58, point moja mbele ya Man City.
Kituko cha Suarez kukwepa kumpa Evra mkono......
No comments:
Post a Comment