22:45 Aston Villa 2-2 QPR
23:00 Blackburn 0-2 Newcastle
23:00 Bolton 0-0 Arsenal
23:00 Fulham 1-1 West Brom
23:00 Sunderland 3-0 Norwich
NB: Saa za Afrika Mashariki
Mechi za leo (ama jumamosi ) ni kipimo cha matokeo ya usajili mdogo uliomalizika 31 Jan.
Newcastle imepanda nafasi ya 6. Msimu huu Arsenal inacheza mchezo wa kinyume nyume (aka mduara),wamepoteza bahati ya kuzoa point tatu muhimu na kuambulia sare. Matumaini ya kumaliza kwenye top four yanaelekea kuwa ndoto za alinacha, na kuna dalili za kumaliza msimu ikiwa chini ya top ten!
Sunderland, Stoke, Everton na Norwich zinahemea nyuma ya mgongo wa Arsenal, kazi ipo msimu huu. Sio kwamba Arsenal awatacheza Champions League msimu ujao, bali hata UEFA ndogo! Matokeo itakuwa kushuka kwa mapato, wanasema tumia pesa kupata pesa, Wenger anaweka talanta chini ya uvungu. Labda miujiza itokee.
Top ten (point kwenye mabano):
1.Man City (54), 2.Man Utd (54), 3.Tottenham (49), 4.Chelsea (42), 5.Newcastle (39), 6.Liverpool (38), 7.Arsenal (37), 8.Sunderland (30), 9.Stoke (30), 10. Everton (29)
No comments:
Post a Comment