Mpambano wa masumbwi kati ya Vital Klitschko (110.5kgs) v Dereck Chisora (109.4 kgs), unaotarajiwa kufanyika leo Olimpiahalle (Munich) nchini Ujerumani umeanza kabla ya muda.
Vital mwenye umri wa miaka 40 anaye shikilia mkanda wa WBC (heavy weight), ameshinda mapambano 43 kati ya 45. Wakati Chisora mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni raia wa Uingereza na mzaliwa wa Zimbabwe, amepambana mara 17 na kushinda 15.
Vital alimpa Chisora nafasi ya kupambana naye kwa heshima kubwa badala ya David Haye, lakini jana Chisora alionyesha makucha yake, kwa kumzaba kibao Vital bila huruma mbele ya umati wa watu wakati wa kupima uzito kwa ajili ya mpambano huo. Labda Vital atajibu mapigo kwenye mpambano leo ili kuthibitisha kwamba 'Kelele za chura........
No comments:
Post a Comment