Sunday 26 February 2012

MECHI YA FINAL- KOMBE LA CARLING - 26 FEB 2012

19:00 Cardif 5-4 Liverpool

NB: Saa za Afrika Mashariki

LIVERPOOL MABINGWA WA KOMBE LA CARLING 2011 /12

Wanasema bahati ya mwenzio.......!

Muda wa Dk 90: Cardif walipata kila nafasi ya kuchukua kikombe, kwanza kwa kupata bao  lililofungwa na J.Mason katika dk ya 18 ya kipindi cha kwanza. Lakini Skrtel akaipatia Liverpool bao la kusawazisha kwenye dk ya 14 ya kipindi cha pili na kufanya sare ya 1-1 hadi mwisho wa dk 90.

Muda wa ziada dk 30: Timu zilimaliza dk 15 za mwanzo bado zikiwa 1-1. Kwenye dk ya 3 ya kipindi cha pili, Kuyt akaipatia Liverpool bao, hata hivyo Turner wa Cardif alisawazisha kwenye dk 12 , na kufanya muda wa zaida kumalizika kwa sare ya 2-2.

Kwenye penalty aka 'Matuta' : inaelekea milingoti ya magoli ilikuwa midogo kuliko kawaida na kusababisha kosakosa kibao akiwemo Gerald, captai wa Liverpool.  Hata hivyo kati ya penalty 5, Bwawa wakapata penalty 3 dhidi ya 2 za Cardif, na hivyo Liverpool kuibuka na kikombe kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 6 iliyopita.

No comments:

Post a Comment