Sunday, 19 February 2012

CHISORA APIGWA NA VITAL, WADUNDANA NA HAYE KWENYE MKUTANO !

Katika pambano la masumbwi lilifanyika jana mjini Munich nchini Ujerumani,Vital Klitschko ameibuka mshindi (119-111, 118-110,118-110) dhidi ya Dereck Chisora, na kuendelea kushikilia mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu wa WBC.

Hata hivyo Waingereza wameendelea kudhihirisha kwamba wao ni maneno mengi nje ya jukwaa la masumbwi.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya mpambano, David Haye aliingilia mahojiano na kusababisha valangati kubwa kati yake na Chisora. Haye amelaumiwa kudhalilisha wana masumbwi wa Uingereza, kufuatia kupoteza mkanda wa WBA kwenye pambano dhidi ya Wladimir Klitschko July 2011 kwa madai kwamba aliumia kinyume na majigambo aliyotoa kabla ya pambano.

Timu ya Chisora ilimtaka Haye kutamka kwamba yuko tayari kupambana na Chisora ili mshindi apambanishwe na Vital. Hatimaye iliishia kuwa vurugu kubwa ya kupigana makonde, huku kocha wa Haye akitokwa damu kwenye paji la uso baada ya kupigwa na chupa!

Ijumaa kabla ya pambano Chisora alimzaba kibao Vital na kuzua vurugu(angalia habari iliyopita ), na alitozwa faini na WBC! Je hatua gani zitachukuliwa kufuatia vurugu za Haye na Chisora?

Valangati lilivyokuwa .............

No comments:

Post a Comment