Tuesday 3 January 2012

WAZIRI MAGUFULI ANASTAHILI KUJIUZULU

Kweli aliyeshiba ..................................!


Ni lini viongozi (Mawaziri wabunge nk) wa Tanzania watawajibika kwa kujiuzulu? Imefika wakati ambapo viongozi wanachukua maamuzi bila kufikiria hathari watakazopata walalahoi.

Waziri wa ujenzi, Mh Magufuli  mara nyingi amekuwa akichukua maamuzi ya kijasiri yenye kuleta mabadiliko mazuri yasiyo tegemewa! Lakini kupandisha nauli za vivuko vya Kigamboni na kuwaambia wananchi wapige mbizi kama awataki kulipa nauli, limeenda kinyume na taratibu kama sio kuvuka mipaka!

Mabadiliko ya nauli nchini huwa yanatangazwa na SUMATRA(  www.sumatra.or.tz ) sababu ndio mamlaka husika. Pia nauli ama garama zozote zile kupanda uambatana na sababu halisi. Na taarifa za garama mpya utolewa mapema. Angalia nchi za wenzetu nauli zimepanda Jan 2012 ( http://www.bbc.co.uk/news/uk-england-london-16379656 ) wakati taarifa zilikadiriwa August 2011 ( http://www.bbc.co.uk/news/uk-14538167 )

Waziri Magufuli ametoa kauli ya kupandishwa nauli badala ya SUMATRA. Tangazo hilo lilitolewa tarehe 29 Dec 2011 bila kuwapa wananchi muda wa kujiandaa. Sababu za kupandishwa kwa nauli ni ubadhilifu ambapo mapato yanakadiriwa kuwa Shs Million 18 lakini yanao kabidhiwa ni Shs million 9. Nauli ikiongezwa si wabadhirifu wataendelea kutajirika!

Kuna Waziri wa zamani wa Fedha aliwahi kutoa kauli kuhusu mabadiliko ya budget, kwamba kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe! Kauli hiyo iliwachefua wengi kama walivochefuliwa wananchi wa Kigamboni. Desturi hii imeota mizizi, na ndio maana hata wabunge wamediriki kujipandishia allowance bila kuwajali wananchi wakiwemo wa Kigamboni.

Wabunge wa Dar es salaam ndio kwanza wanaibuka usingizini na kuwatetea wananchi wa Kigamboni ( http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/18995-wabunge-dsalaam-wamvaa-magufuli.html ) , walikuwa wapi siku zote nauli zikipanda kiholela msimu wa sikukuu? Nao Waheshimiwa Wabunge wa mikoani wamewajibika vipi, mfano nauli za Arusha - Dar zimepanda toka 18,000 mpaka 30,000 msimu huu wa sikukuu! Ama wanapata viyoyozi kwenye mashangini ( a.k.a magari ya kifahari) na kuwasahau wapiga kura wao.

Waziri Magufuli sio tu aombe radhi kama wanavyodai wabunge wa Dar es salaam, bali ajiuzulu, ili iwe mfano kwa viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment