Wednesday, 4 January 2012

MECHI ZA 04 JAN 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

23:00 Everton 1-2 Bolton
23:00 Newcastle 3-0 Man Utd

NB: Saa za Afrika Mashariki

-JAHAZI LAENDELE KUZAMA- Man Utd ilipigwa 3-2 na Blackburn  mechi ya kufunga mwaka, wameendelea na dose kwa kupewa kipigo kwenye mechi ya kufungua mwaka , sasa Tottenham wananyemelea nafasi ya pili, wakati Man City wakiendelea kupaa!

Newcastle ilifungwa 3-1 na Liverpool  mechi iliyopita, wamepunguza maumivu leo, sasa wananyemelea nafasi ya nne kama sio top six! Liverpool, Arsenal na Chelsea matumbo joto!

-Bolton walikuwa wanashika mkia (nafasi ya 20) kabla ya mechi ya leo, ushindi ume wamesogeza nafasi  ya 18! Huu msimu autabiriki!


-Mechi zinazofuata ni za FA Cup(baadhi ya mechi muhimu)- Liverpool v Oldham (Ijumaa 6 Jan, saa 23:00), Man Utd v Man City, Chelsea v Portsmouth ( Jumapili ,8 Jan), Arsenal v Leeds (Jumatatu, 9 Jan),

-Premier league itaendelea 11Jan


No comments:

Post a Comment