Sunday, 29 January 2012

WAKAGUZI WA MITAMBO YA NUCLEAR WAMEWASILI IRAN

Mwenye nguvu............!
Wawakilishi wa kimataifa  wa nguvu za Atomic (IAEA - International Atomic Energy Agency) wamewasili nchini Iran kwa ziara ya siku tatu, kuanzia leo 29 Jan  mpaka 31 Jan  kukagua mitambo ya nuclear.

Nia ya ziara hiyo ni kuthibitisha madai ya Iran kwamba inatumia mitambo ya nuclear kwa shughuli za maendeleo na sio uzalishaji wa silaha za nuclear.

Iran inatakiwa kutoa ushirikiano na kujibu maswali yote kwa wakaguzi hao, ili kumaliza mzozo kati yake na Nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani, mzozo ambao umesababisha vikwazo dhidi ya Iran(kujua zaidi angalia- MGOGORO WA IRAN WABADILI MWELEKEO ).

Mwakilishi wa Iran kwenye IAEA amesema matokeo ya ziara hiyo yatafichua njama za nchi  za magharibi dhidi ya Iran. Na mkuu wa IAEA amesema anatumaini ziara hii itamaliza mzozo uliopo.

Rais wa Iran amesema yupo tayari kukutana na nchi za magharibi kwa mazungumzo ili kutatua mgogoro kati ya pande hizo.

Yote haya ni matokeo ya vikwazo. Je wakaguzi hao watagundua nini? Na rais wa Iran atakutana lini na kuafikiana nini na mataifa ya Magharibi? Ama hizi ni harakati za Iran kuchelewesha vikwazo. Marekani awajasahau Drone yao!

No comments:

Post a Comment