Saturday, 7 January 2012

MPAMBANO WA AMIR KHAN V LAMONT WAZUA UTATA

Muda umepita tangu kufanyika mpambano huo wa masumbwi kati ya Amir Khan na Lamont Peterson, ambapo Lamont alishinda

Baada ya pambano hilo  lililofanyika Washington DC tarehe 10 Dec 2011, Amir alilalamika kuhusu upendeleo uliofanywa na msimamizi wa pambano hilo, jambo lililochangia kupoteza mikanda yake WBA na IBF.

Wakati juhudi za kutaka mpambano huo urudiwe zinaendelea, utata umejitokeza baada ya kambi ya Amir kugundua mapungufu yaliyojitokeza  kama ifuatavyo :-

-Mtu asiyestahili alikaa katika nafasi ya judge, aliondolewa lakini baadae alirudi na kufanya idadi ya judges kuwa wanne badala ya watatu.

-Mtu huyo alikuwa akitoa maelekezo kwa judges, kinyume na taratibu hivyo kuingilia maamuzi ya judges.

-Vijikaratasi vilitolewa na mtu huyo na kuelekezwa kwa judges wote kinyume na taratibu.

-Matokeo ya mshindi yalichukua muda kutolewa.

-Mtu huyo alijumuika na timu ya Lamont wakishangilia ushindi.

Timu ya Amir Khan inasubiri ufafanuzi kuhusu mtu huyo toka kwa shirikisho la ngumi. Ili kujua na kushangaa zaidi angalia ..........

No comments:

Post a Comment