Saturday, 28 January 2012

MECHI ZA 28 JAN 2012 - KOMBE LA FA UINGEREZA

15:00 QPR 0-1 Chelsea
15:45 Liverpool 2-1 Man Utd
18:00 Bolton 2-1 Swansea
20:15 Brighton 1-0 Newcastle

NB Saa za Afrika Mashariki

-Ni baadha ya mechi za kombe la FA zinazousisha miamba vya premier ligi.

-Mechi ya QPR na Chelsea ilikuwa ya kukata na shoka, sio ndani bali kabla ya mechi! Chanzo ikiwa ni songombingo lililozuka kwenye mechi ya Oct 2011 miamba hii ilipokutana ambapo utata ulizuka kati ya John Terry (captain wa Chelsea) na Anton Ferdinand (mdogo wake Rio Fedinand). Terry alishutumiwa kutumia maneno ya ubagizi wa rangi (racism) dhidi ya Ferdinand na kesi itaunguruma rasmi mahakamani Jumatano ijayo.

-Lakini munkari wa washabiki wa QPR na Chelsea ulibidi kutulizwa kwa kuondoa jadi ya wachezaji kupeana mikono kabla ya mechi na ulinzi mahiri kufuatia barua aliyotumiwa Ferdinand yenye risasi, na uchunguzi unaendelea. Naye Ferdinand anasemekana kutumia fedha kibao kujilinda na uhasama wowote ule!

-Hatimaye Chelsea wameibuka kidedea kwa kuwabamiza QPR! Je nani atashinda mechi ya mahakamani????????!!!!

-Bila Kusahau kinyongo baina ya mashabiki wa Liverpool v Man Utd kufuatia Luis Suarez kufungiwa mechi nane dhidi ya kauli zake ubaguzi wa rangi alizotoa dhidi ya  Evra!

-Liverpool ilitoa kipigo kwa Man City kombe la Carling wiki hii. Na leo wametumia nafasi vizuri kwa kutembeza kipigo kwa Mashetwani Wekundu aka Man Utd! Ahhhhhh, Bwawa la maini nao, wanaona utaaamuuu!!!!!!

-Swansea nao wanaona uchunguuuuu, nadhani wanajutia ushindi wa ile mechi dhidi ya Arsenal!

-Kesho- Arsenal v Aston villa (19:00), Sunderland v Middlesbrough (16:30)

No comments:

Post a Comment