Kuna utata unaojitokeza wakati viongozi wa serikali wakiwa kwenye ziara nchini ama nje ya nchi. Sijui kama ni halali ama la!
Viongozi wa serikali wakiwa kwenye ziara za kiserikali, gharama zao zinalipwa na serikali kupitia kodi za wananchi wote bila kujali itikadi ya chama, na jambo hilo halina utata wowote.
Viongozi wa serikali wakia kwenye ziara za vyama vyao ni dhahiri garama zinalipwa na vyama vya husika, hili nalo linaeleweka vizuri.
Utata unakuja pale viongozi wa serikali wakiwa kwenye shughuli za serikali wanapochanganya shughuli za vyama (kisiasa), garama hizi zinalipwa na nani?
Mfano mzuri ni terehe 20 Jan 2012, Makamu wa Raisi alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Chiumbata, Nachingwea Mkoa wa Lindi. Katika mkutano Makamu wa Rais alipokea kadi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA aliyeamua kujiunga na CCM. Pia mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi alihutubia ( twanga hapa- http://michuzijr.blogspot.com/2012/01/makamu-wa-rais-dkt-bilal-atembelea.html#comments )
Swali ni nani anagharamia ziara hiyo? Je katiba inasemaje kuhusu swala hilo? Je Vyama vya upinzani vimegundua hilo na Mawaziri vivuli wanafuatilia gharama za ziara kama hizo?
Katika mfumo wa vyama vingi ni vizuri kutenga shughuli za chama na serikali, ili kuweka bayana swala la gharama.
No comments:
Post a Comment