Wednesday, 25 January 2012

MGOGORO WA IRAN WABADILI MWELEKEO

Iran imelaani vikwazo vilivowekwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) dhidi ya Iran. Vikwazo hivyo ni harakati za kuishinikiza Iran kusitisha mipango yake ya kuzalisha silaha za nuclear. Kabla ya vikwazo hivyo Iran ilidai uchumi wake autaathirika kwa namna yoyote.

Nchi wanachama wa umoja wa EU zinatakiwa kusitisha uagizaji wa mafuta yasiyosafishwa na bidhaa zake toka Iran, pia kusitisha mikataba yote ifikapo 1 July 2012. Hatua hizi ni kama kupigilia msumari mwingine kufuatia vikwazo vilivyopitishwa na Marekani dhidi ya Irani ( kujua zaidi angalia- MZOZO KATI YA IRAN NA MAREKANI UNAELEKEA PABAYA ).


Kuna walakini kama vikwazo vya Nchi za EU vitafanikiwa, sababu Iran inauza asilimia 20 tu ya mafuta yake kwa nchi za EU ukilinganisha na kiasi inachouza nchi za Asia (China 20%, Japan 17%, India 16% ). Juhudi zinafanywa ili kuzishawishi nchi za Asia kusitisha uagizaji wa mafuta toka Iran ( http://www.bbc.co.uk/news/world-europe-16678342 )


Mwishoni mwa mwaka jana Iran ilidai itafunga eneo/ lango la bahari (Strait of Hormuz) kama vikwazo vitawekwa dhidi yake. Eneo hilo ni muhimu kwa nchi za eneo hilo kwa kusafirisha mafuta. Iran ilifanya mazoezi ya kivita eneo hilo la bahari kufuatia vikwazo vya Marekani. Jumatatu ya wiki hii meli za kivita za Marekani, Uingereza na Ufaransa zimepita eneo hilo bila madhara.


Matokeo ya vikwazo yameanza kuonekana kwani Iran imechukizwa na kudai vikwazo hivyo ni uonevu na sio haki (http://www.bbc.co.uk/news/world-europe-16693484 ) . Bei ya mafuta imepanda katika soko la dunia, na fedha ya Iran imeshuka thamani. Pia inadhaniwa kutoelewana kati ya Iran na nchi jirani kutatokea, jambo ambalo litaathiri zaidi bei ya mafuta katika soko la dinia.

Ili kutatua mgogoro Iran inatakiwa kusitisha mipango yake ya salaha nuclear na kufanya mazungumzo na nchi za EU na Marekani. Kama Iran itazuia eneo hilo la bahari vita avitakuwa mbali.

No comments:

Post a Comment