Tuesday 6 December 2011

VUGUVUGU ZA KISIASA RUSSIA ZINAPAMBA MOTO

Kati ya nchi zisizo na masikio ya kusikia ama macho ya kuona  kitu kinachoitwa democrasia ya kweli, basi Rusia lazima itakuwa inaongoza kwenye msimao wa league hiyo.

Shirikisho la USSR (1922-1991) lilikuwa mwamba mgumu, ulioweza kuipa USA upinzani wa hali ya juu mpaka 1991 shirikisho hili lilipo pukutika! Kilichofuata ni nchi ya Russia kuibuka na kuendeleza gurudumu lililiachwa na USSR.

Nani angetegemea kuona kiongozi wa Russia akizomewa hadharani? Basi ukisikia democrasia inapiga hodi Russia, uenda muda si mrefu mambo yatakuwa tofauti. Dalili zinajionyesha kufuatia chama tawala (United Russia) kupoteza idadi kubwa ya viti bungeni kwa kupata chini ya 50% ukilinganisha na uchaguzi uliopita! Inasemekana ni dalili kwamba wananchi wanapinga mpango wa waziri mkuu Putin wa kutaka kugombea urais March mwakani.

Waziri mkuu Putin amekumbwa na upinzani wa wazi, ikiwemo kuzomewa hadharani ( http://www.youtube.com/watch?v=nS48UuVXbjQ ) . Pia maandamano kupinga ushindi wa United Russia yamerindima wiki hii ambapo kiongozi wa upinzani na watu zaidi ya 250 wamekamatwa. Hata hivyo wapinzani wanaendeleza harakati za kufanya maandamano zaidi kwa kutumia mtandao wa face book kwa jina-  ''Is the Revolution Continuing? Yes!''

Marekani imeishutumu serikali ya Russia kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi ambao umesaidia chama cha United Russia kushinda, lakini serikali ya Russia imepinga madai hayo. Je,Waziri mkuu Putin atajipanga vipi ili kushinda uchaguzi wa March mwakani?

Inafahamika kwamba, Russia ni mpanzani mkuu wa USA, ambapo nchi kama Syria, Iran, Cuba, China n.k zinaunga mkono mikakati ya Russia (aka kiranja wao) katika kushindana na USA.

Swali: democrasia kuweka mizizi Russia ni kazi ya USA katika kuporomosha mwamba huo na washiriki wake? Wanasema polepole..........!

No comments:

Post a Comment