Wednesday 16 November 2011

RAIS ROBERT MUGABE AMEONYESHA MFANO GANI ?

Pamoja na hali ngumu ya maisha inayo kabili jamii nyingi katika bara la Africa, viongozi wengi wanakula na kusaza bila aibu.

Mfano mzuri ni raisi Robert Mugabe  wa Zimbabwe,bila aibu amehudhuria graduation ya mwanae katika City University nchini Hong Kong, akiwa anaelekea kwenye ziara yake nchini China (http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-china-15751359 ).

Inaonyesha kiasi gani viongozi wetu awana huruma na jamii zetu masikini ambazo azina uwezo wa kusomesha watoto sio nje ya nchi tu, bali hata ndani ya nchi.  Jamii nyingi hazipati huduma na mahitaji muhimu kama chakula, malazi, matibabu, elimu  ya msingi nk!

Viongozi wetu wanadiriki kutumia kodi za walala hoi na misaada toka nje ya nchi kusomoshea watoto wao nje ya nchi huku familia nyingi masikini zinataabika! Tanzania ni mojawapo ambapo viongozi wanapata huduma za matibabu na kusomesha watoto wao nje ya nchi!

Shame up on all African leaders!

No comments:

Post a Comment