Sunday 27 November 2011

MSIMU WA FORMULA 1 WAMALIZIKA

Msimu wa yale magari (Sport Cars) yenye kasi ya ajabu, bei kubwa na yanayotumia technologia ya hali ya juu umemalizika. Ni Formula 1 namaanisha!

Katika ngwe ya mwisho iliyofanyika Interlagos (Brazil) sio wenyeji Felipe Massa ambaye alimaliza nafasi ya tano, ama Reuben Barrichello(aliyemaliza wa 14) waliofanikiwa kuwafurahisha wenyeji wao, wala sio Vetel aliyezoea kushinda race zote za msimu kuendeleza mapigo!

Lakini kama ilivyozoeleka team Redbull (Vetel na Webber) kushinda ni Mark Webber aliyefanikiwa kushika nafasi ya kwanza huku Vetel akijikokota na kushika nafasi ya pili na kumwaangalia Button akishika nafasi ya tatu, ambapo team Ferari waliwezeshwa na Alonso kushika nafasi ya nne akimtangulia mwanzake Felipe Massa aliyeshika nafasi ya tano.

Balaa likiendelea kumwandama Lewis Hamilton baada ya kushindwa kumaliza race hizo baada ya mkoko wake kuharibika gear-box na hivyo kulazimika kujitoa na kubakia kuwa mtazamaji.

Msimu umekwisha tugange yajayo ambapo msimu mwingine utaanzia nchini Australia 17/18 March 2012 


No comments:

Post a Comment