
picha kwa hisani ya www.michuzijr.blogspot
CHADEMA wamefanikiwa kilio chao kusikilizwa kuhusu katiba mpya baada ya jana kukutana na JK ambapo mazungumzo yataendelea leo!
Sio tu kwa faida ya CHADEMA bali ni kwa faida ya vyama vingine vya upinzani na wananchi kwa ujumla. Lakini huo sio mwisho wa kupigania kupata katiba yenye kuwakilisha mawazo ya Watanzania wote bali ndio mwanzo, kwani mapendekezo hayo yanaweza kutiwa kapuni na JK na serikali yake mara baada ya CHADEMA kuipa kusigo ikulu.
Kama mapendekezo ya CHADEMA yamejumuisha mawazo ya vyama vingine vya upinzani huu utakuwa mwanzo mzuri, lakini kama vyama vingine vya upinzani avijaridhia mapendekezo yaliyotolewa na CHADEMA na yale ya muswada uliopitishwa na bunge, basi inabidi rais Kikwete kuvipa nafasi vyama vingine vya upinzani kutoa mapendekezo yao ili kundoa dukuduku zao.
Wananchi hatujui nini kilichopo kwenye mapendekezo CHADEMA na yale ya muswada wa bunge aliopewa JK! Wananchi tunahitaji kufahamishwa na sio viongozi wenyewe kubania kwapani maswala yanayohusu wananchi.
Kwa hatua iliyofikiwa, Bunge limeonyesha udhaifu mkubwa kwani yote haya yangestahili kufanyika bungeni na muswada unfikishwa kwa rais katika hatua ya mwisho. Pia hatua hii iliyofikiwa imeonyesha mianya iliyopo kwenye uongozi wa bunge la Tanzania kuhusu upendeleo kwa chama tawala na kutotaka kusikiliza vyama vya upinzani wanapotoa mawazo yao.
Nini kitaafikiwa kwenye mkutano wa leo kati ya JK na CHADEMA? Hatujui sababu hatujui nini kipo kwenye makabrasha yao, tupo gizani tuelekeze macho na masikio ikilu!
kwa taarifa za kuthibitisha kikao hicho twanga hapa - http://issamichuzi.blogspot.com/2011/11/rais-kikwete-akutana-na-uongozi-wa.html
No comments:
Post a Comment