Saturday 8 October 2011

YALIYOJIRI KWENYE FOMULA 1

Japanese Grand Prix
Qualifying -Matokeo  (top 7) - 1.Vetel  2.Button 3.Hamilton 4.Massa 5.Alonso 6.Webber  7.Schumacher

Hamilton kama ilivyo kawaida msimu huu, alichelewa kwa sekunde chache kuanza mzunguko wa mwisho kutetea nafasi ya kwanza (pole position) ambayo alinyakuliwa na Vetel na baadae Button kuchukua nafasi ya pili hivo Hamilton kusukumwa nafasi ya tatu, kwani kabla  ya hapo alikuwa nafasi ya kwanza ambayo ingempa nafasi nzuri kushinda kesho.

Je Hamilton atarudia kosa kama la leo hapo kesho, na tukumbuke kwamba Massa yupo nyuma yake, uenda yaliyotokea Singapore yakazuka tena (kwa undani pitia  habari ya hapo chini)! Vetel akishinda ama kupata point moja kesho atachukua ubingwa wa msimu huu ikiwa bado kuna ngwe (races) nne za kukamilisha msimu. Je Button atakubali kushindwa kesho, kwani kama atashinda na Vetel asipate point yoyote kutachelewesha Vetel kuchukua ubingwa wa msimu huu.

Tusubiri kesho, kwani kwa ushindani uliopo uenda chochote chaweza kutokea!


No comments:

Post a Comment