Monday 30 April 2012

MECHI ZA 30 APRIL 2012 - LIGI KUU YA UINGEREZA

22:00 Manchester City 1-0 Manchester United

NB: Saa za Afrika Mashariki

Ingekuwa ile timu ya nanii wangeanza kuimba:- Wameinama.......,Wameinuka..., wanaona haya haooo!


Kwanini Man City wame wanyanyasa Man Utd hivyo? Awaoni huruma Rooney analia? 

Ferguson naye alipandisha mzuka dhidi ya Mancini........

Man City inaongoza ligi ikifuatiwa na Man Utd, zote zikiwa zina point 83 na mechi 2 kumalizia msimu!

Mechi zao zilizobaki:
6 May:- Newcastle v Man City, Man Utd v Swansea

13 May:- Man City v QPR,  Sunderland v Man Utd


---------------------------------------------------------------------------------------------------
Leo ni leo, nani ataibuka na point 3, ama ni sare?

Man Utd inaogoza ligi ikiwa na point 83. Ushindi utaongeza tofauti ya point kuwa 6 dhidi ya Man City.

Man City inashikilia nafasi ya 2 ikiwa na point 80, ikishinda itafikisha point 83 sawa na Man Utd na kusogea kwenye nafasi ya kwanza.

Baada ya mechi hii Man City na Man Utd zitakuwa zimebakiza mechi 2 kila moja, kukamilisha msimu!

No comments:

Post a Comment