Thursday 6 October 2011

JE WEWE NI MSHABIKI WA FOMULA 1 ?

Kama ni mshabiki wa Fomula 1 tupo pamoja, na kama sio mshabiki basi ujachelewa, jaribu kufuatilia na muda si mrefu utafaidi uhondo.

Ngwe inayufuata itakuwa Japan weekend hii kama ifuatavyo (kwa time za Afrika Mashariki):-
Friday 07 Oct 2011: Practice 1: saa10:00 - 11:30 ( usiku wa kuamkia kesho) na  Practice 2: saa 02:00- 09:30 ( kesho asubuhi)

Saturday 08 Oct 2011: Practice 3: saa 11:00 -12:00 (asubuhi) na Qualifying saa 02:00-03:00 (asubuhi)

Sunday 09 Oct 2011: Race -saa 03:00 asubuhi

Race zilizopita za Singapore hali ilikuwa sio shwari kwa driver Hamilton kwani ni kama  msimu huu mambo yanamwendea mrama. Kikubwa zaidi ni pale Hamilton alipomgonga Massa wakati akitaka kumpita http://www.youtube.com/watch?v=WfKZ81DdM2Y . Habari zilizozuka wiki hii zinadai wakati race zinaendelea Massa aliamriwa na boss wake kuhakikisha anamzuia Hamilton asimpite ( hold Hamilton as much as we can', 'destroy his race as much as we can, come on boy' ), kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.

Kama desturi baada ya race madereva huwa wanahojiwa na waandishi wa habari, hapo kilizuka kituko kwani Massa alionyesha wazi hasira zake alipovuruga mahojiano ya Hamilton na waandhishi wa habari, na kumwambia Hamilton 'good job, well done', Hamilton alimjibu usiniguse (' dont touch me') http://www.youtube.com/watch?v=SKjaBdCaJ5k&feature=related .

Kwa mzozo huu tusubiri ngoma itakuwaje Japan weekend hii, Je Hamilton na Massa watasuluhisha tofauti zao? Je Hamilton atapata matokea mazuri ama atavurunda? Kwani alikuwa na nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa mwaka huu lakini hiyo imekuwa ndoto kwa sasa.

No comments:

Post a Comment