Idara mbali mbali za serikali na binafsi, sinapaswa kuiga na kujifunza mengi kutoka nchi zenye uzoefu.
Mfano swala la kupandisha gharama mbalimbali zikiwemo umeme, mafuta, usafiri nk. Tanzania kupanda kwa bei hizo uwa ni kama zima moto, raia awapewi muda wa kujiandaa ama kujadili mabadiliko yanayofanywa bali ushtukizwa . Mfano mzuri ni mabadiliko bei ya za mafuta zilizotokea hivi karibuni,kisingizio ni Inflation!
Mabadiliko ya bei yanayofanywa kwa kushtukizwa huwa yanaathiri sio tu watumiaji haswa wenye vipato vya chini bali hata wafanyabiashara kwa namna moja ama nyingine.
Angalia jinsi wenzetu matajio ya bei za nauli za train yanayotarajiwa mwakani, taarifa imetolewa leo, na sababu ni Inflation - http://www.bbc.co.uk/news/uk-14538167
Je idara husika Tanzania zinawajibikaje katika hili, ukichukulia kwamba mabadiliko ya bei ghafla yanaleta madhara kama ilivotokea mgomo wa wauzaji mafuta ulioleta mateso kwa wananchi, na pia kuikosesha serikali mapato?
Je nani anawajibishwa kutokana na hasara na mateso yaliyojitokeza kufuatia mgomo ule wa wauzaji mafuta?
Majibu yote haya nina hakika yatapatikana kama wahusika ni wawajibikaji.
No comments:
Post a Comment