Budget ya Wazara ya Nishati na madini ilikataliwa bungeni kutokana na budget hiyo kutokuwa na mikakati ya uhakika ya kumaliza tatizo la umeme nchini.
Wakati budget hiyo ikitafutiwa ufumbuzi, ulizuka mgomo wa vituo vya mafuta baada ya EWURA kushusha bei ya mafuta kinyume na matarajio ya wauzaji hao. EWURA ililazimika kuitisha kikao cha wauza mafuta na baada ya hapo vituo hivyo vilianza uuzaji wa mafuta isipokuwa BP ambao walifungiwa.
Wakati EWURA ambayo ni sehemu ya Wizara ya Madini na Nishati ikiendelea kuyabana makampuni ya mafuta, Wizara ya Nishati na Madini walirudisha budget bungeni baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyosisitizwa na Waheshimiwa Wabunge na kupitishwa bila ya kujua nini kitafuata baada ya hapo.
Leo hii bei ya mafuta imepandishwa,tujiulize ni kwanini tukio hili limefanyika wakati budget imeshapitishwa? Ieleweke kwamba kama tatizo la mafuta lisingetatuliwa ingeongeza kikwazo kingine kwa budget ya Wizara ya Madini na Nishati.
Mabadiliko ya bei :-
03/08/11(punguzo) 15/08/11(ongezeko) Tofauti
Petrol -Tsh 202.37 Tsh 100.34 Tsh 102.03
Diesel -Tsh173.49 Tsh 120.47 Tsh 53.02
Mafuta Taa -Tsh 181.37 Tsh 100.87 Tsh 80.50
Kwa ujumla bei zimepungua ukiachilia mbali badiliko la kwanza, ingawa imepunguza furaha za wananchi na wabunge ukilinganisha na badiliko la tarehe 03/08/11
Hiyo ilikuwa kiini macho kwa wabunge na wananchi. Serikali nabidi itoe maelezo kwa wananchi. Kwanini tukio hili linatokea baada ya budget kupitishwa, na ni mpaka lini wananchi tutaendelea kuteseka na kubebeshwa mzigo wa tatizo la umeme, mafuta nk.
Kama kushuka kwa thamani ya Tsh ndio sababu, mbona thamani imeshuka muda mrefu na awakufanya hivo, iweje thamani ishuke katika siku chache na bei ya mafuta iongezwe?
Je kuna uzembe na nani atawajibishwa? Je miaka 50 ya uhuru tunasherehekea matatizo ama mafanikio?
for more- http://mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/14505-serikali-yapandisha-tena-bei-ya-mafuta.html
No comments:
Post a Comment